Kizaazaa kilizuka katika mahakama ya Malindi nchini Kenya siku ya Jumatano wakati mwanamume anayekabiliwa na mashtaka ya ulaghai alipoanza kupiga kelele akiitaja mahakama kuwa isiyofaa zaidi duniani.
Carlos Taka, 68, anashtakiwa kwa makosa sita ya kujipatia pesa kwa kujifanya kuwa afisa wa umma.Malalamishi yake yalichochewa na uamuzi wa hakimu kuahirisha kesi yake kwa mara ya kumi na moja.
"Nimekaa rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa sababu tu baadhi ya mashahidi walishindwa kutoa ushahidi. Hii ndiyo mahakama isiyo na manufaa yoyote duniani," alisema na kubainisha kuwa kucheleweshwa kwa haki ni sawa na kunyimwa haki.
Kizaazaa kilizuka katika mahakama ya Malindi siku ya Jumatano wakati mwanamume anayekabiliwa na mashtaka ya ulaghai alipoanza kupiga kelele akiitaja mahakama kuwa isiyofaa zaidi duniani.
Carlos Taka, 68, anashtakiwa kwa makosa sita ya kujipatia pesa kwa kujifanya kuwa afisa wa umma.Malalamishi yake yalichochewa na uamuzi wa hakimu kuahirisha kesi yake kwa mara ya kumi na moja.
"Nimekaa rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa sababu tu baadhi ya mashahidi walishindwa kutoa ushahidi. Hii ndiyo mahakama isiyo na manufaa yoyote duniani," alisema na kubainisha kuwa kucheleweshwa kwa haki ni sawa na kunyimwa haki.
Anadaiwa kuwa mnamo Septemba 21, 2021 katika Mahakama ya Kale ya Malindi, alijiwasilisha kwa uwongo kama mfanyakazi wa Utumishi wa Umma kwa Mary Masisa.