Moto wazuka mlima Kilimanjaro

Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana, umezuka katika mlima Kilimanjaro, karibu na eneo la Karanga Camp lililopo urefu wa meta 3,963 kutoka usawa wa bahari kupitia njia ya Mweka na jitihada ya kuuzima zinaendelea.

Moto huo ulianza kuonekana jana Oktoba 21, 2022 usiku kutokea Moshi Mjini, ambapo Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi Tanzania (Tanapa), William Mwakilema aliyezungumza na Mwananchi leo Oktoba 22, amesema vikosi vinaelekea kuuzima moto huo.


Taarifa zinaeleza moto huo unawaka ukanda wa Moorland, ambao mimea yake ikishika moto huwa ni mkali na tayari Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) na Hifadhi ya Kilimanjaro (Kinapa) wametuma vikosi kwenda kuukabili.


chanzo:mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo