Mwanamke mwenye umri wa miaka 22 alishtakiwa Ijumaa kwa kumtupa mtoto wake mchanga kwenye mto Chania kaunti ya Nyeri nchini Kenya
Elsie Makena alikabiliwa na shtaka la kujaribu kuua mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mercyline Lubia.
Mahakama ilisikia kwamba tukio hilo lilitokea mwendo wa saa kumi na mbili jioni siku ya Jumatano.
·
Lakini mvulana huyo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba aliokolewa na msamaria mwema dakika chache baadaye.
“Mtoto huyo amechukuliwa na nyumba ya watoto mjini kwa usalama wake,” ilisema ripoti ya polisi iliyotolewa mahakamani.
Bi Makena alikanusha shtaka hilo na kuomba masharti nafuu ya bondi.
Hakimu Lubia alimpa bondi ya Sh1 milioni na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itaendelea Novemba 8.