Uongozi wa klabu ya Yanga umeandaa tukio la kumpongeza kocha wake Nasridine Mohamed Nabi pamoja na benchi lake la ufundi kwa kukiongoza kikosi hicho kucheza mechi 43 za ligi kuu bila kupoteza mchezo hata mmoja.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, tukio hilo linafanyika leo katika mchezo wao dhidi ya KMC, ambapo itakapofika dakika ya 43, mashabiki watasimama na kumpigia makofi kocha huyo.