Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa jumuiya ya vijana CCM wilaya ya Makete ndugu Ellymathew Kika amewataka vijana kulijenga na kulilinda Taifa lao Ili kujiletea mandeleo na usalama wao binfsi.
Kika ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na wanahabari kuelekea kilele cha siku ya vijana pamoja na kumbukumbu ya miaka 23 tangu kutokea kifo Cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Amesema ni vyema wakatambua nafasi Yao katika ujenzi wa taifa lao badala ya kusubiri watu wachache wawaaamulie namna taifa linapaswa kuwa.
"imekuwa kawaida Kwa vijana wetu kutokuhoji Wala kushauri mipango ya serikali na baadaye wanageuka kuwa walalamikaji wa maamuzi hayo,Ni vyema sana vijana kuanzia ngazi ya mtaa Hadi taifa kushiriki mikutano,makongamano na midahalo yote muhimu inayolenga kupokea maoni na mawazo mapya ya kujenga nchi yetu"
Aidha Kika amewataka vijana kushirikiana vizuri na viongozi wa kuchaguliwa ili waweze kuyafikisha mawazo Yao.
"Niwasihi vijana Kwa Yale mambo ya kisela wanayohisi na kuona yanahitaji maboresho,ni vyema sana wakafikisha mawazo Yao Kwa wenyeviti wa mitaa/vijiji,madiwani na Mbunge Ili wayafikishe kwenye vikao vya maamuzi".
Pia Kika amewasisitiza vijana kujishughulisha na kazi za uzalishaji ili kujipatia kipato halali na endelevu na hatimaye wawe sehemu ya walipa Kodi ya maendeleo ya Taifa letu.
"tunaposubiri serikali itengeneze mazingira mazuri Kwa vijana yatokanayo na mawazo ya vijana wenyewe, ni vyema nasisi vijana tukaendelea kufanya kazi halali ili tuweze kujipatia kipato na kushiriki kuchangia Pato la taifa".
Akimzungumzia Hayati Baba wa Taifa,Kika amewataka vijana kusoma machapisho na kufatilia hotuba za Mwalimu Nyerere Kwa ukaribu kwani zitawaongezea ujasiri wa kulipambania taifa lao.
"Katika Umri wa miaka 27 tu Mwalimu alishaaminika kuiendesha nchi yetu tena katika kipindi ambacho hatukuwa na wasomi wengi Wala uchumi wa taifa haukuwa sawa, tukitafuta vitabu vinavyomzungumzia mwalimu na kusikiliza hotuba zake zitatutia hamasa vijana kushiriki na kuingia katika nafasi za kiuongozi katika jamii zetu na kuonyesha vipawa vyetu".
Pia ameiomba serikali kuendelea kitengeneza fursa nyingi ambazo zitawanufaisha vijana kiuchumi pamoja na kuendelea kutoa ajira Kwa vijana wenye taaluma mbalimbali.