Mahakama ya Shanzu katika kaunti ya Mombasa Kenya imemhukumu mwanamume mwenye umri wa miaka 21, kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanamke aliye na ugonjwa wa akili.
Katika hukumu yake, Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Shanzu Yusuf Shikanda, alibainisha kuwa kitendo alichofanya Dickson Joshua dhidi ya mwanamke huyo mwenye ulemavu wa akili na asiye na hatia kilikuwa cha kinyama.