IGP ataka uchunguzi wa kina mauaji ya watu Morogoro

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura ameagiza kufanyika kwa uchunguzi kufuatia mauaji ya Watu wawili yaliyosababishwa na vurugu zilizoibuka jana katika Kijiji cha Ikwambi, Morogoro baada ya Wakulima kuwafungia Ofisini Viongozi na Wafugaji na kutaka kuwachoma moto.


IGP Wambura akiwa Dar es salaam amesema Polisi walifika Kijijini hapo kutuliza vurugu ambapo kulitokea tafrani iliyosababisha matumizi ya mabomu na risasi za moto “Wananchi wa Kijiji cha Ikwambi wawe watulivu na watoe ushirikiano wakati Timu itakwenda kufanya uchunguzi”

“Pili kwa upande wa Jeshi la Polisi nimeelekeza Askari wote waliohusika kwenye tukio hilo wapishe uchunguzi wakae kando, endapo itabainika mapungufu au madhaifu au chochote kile ambacho kinaonesha uzembe kwa upande wa yeyote yule basi hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake”

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa amesema tukio hilo limetokea October 23,2022 ambapo chanzo ni Wakulima kuwafungia ndani ya Ofisi Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji pamoja na Wafugaji kwa lengo la kutaka kuwachoma moto baada ya kudai Viongozi hao wameshindwa kuwasaidia mashamba yao yanapovamiwa na Wafugaji na kulisha mifugo yao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo