15 washikiliwa na polisi kwa kumkata masikio Mkulima

Jeshi la polisi wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro linawashikilia watu 15 kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumkata masikio Fabian Mkuti mkulima mkazi wa kijiji cha Libenanga kata ya Mwaya wilayani humo.


Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa Wasafi Media, Mkuu wa wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya amesema tukio hilo limetokea usiku wa Oktoba 9 mwaka huu katika kijiji cha Libenanga.

Malenya amefafanua kuwa chanzo cha tukio hilo ni mabishano kati ya wafugaji na mkulima ambaye alikuwa anazuia Ng'ombe kuingia shambani.

Malenya ameeleza kuwa kufuatia tukio hilo yeye na kamati ya ulinzi na usalama walianza kufanya oparesheni usiku huo na kufanikiwa kukamata Ng'ombe 300 na wafugaji 15.

Baada ya tukio hilo majeruhi huyo alikimbizwa katika katika kituo cha afya Mwaya ambapo anaendelea na matibabu.

Watuhimiwa hao wanashikiliwa katika kituo cha polisi Mahenge na upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakani.

Chanzo: Wasafi media


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo