Wanaume wauana Mtwara wakigombania Penzi

Watu wawili waliotambulika kwa majina ya Ibrahimu Shaban (21) na Musa Bakari (28) wamefariki dunia wilayani Masasi mkoani Mtwara, baada ya kupigana kwa kutumia magogo wakati wakigombea mpenzi wao aitwaye Khadija Msamati.


Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi ACP Nicodemus Katembo amesema tukio hilo limetokea jana Septemba 29, 2022 majira ya saa sita usiku katika kijiji cha Mkangaula kata ya Namalenga wilayani Masasi.

ACP Katembo amesema tukio hilo limesababishwa na wivu wa mapenzi na baada ya kufanyika kwa uchunguzi wamebaini marehemu hao walikuwa kwenye ugomvi wa kugombea mpezi wao ambaye baada ya tukio hilo alitoweka na kwenda pasipojulikana.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo