Watu watano ambao ni washukiwa wa matukio ya ujambazi wameuawa baada ya kukaidi amri ya askari walipokuwa wakijiandaa kuvamia kiwanda cha Daazhong eneo la changarawe Mjini Mafinga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema washukiwa hao waliuawa baada ya kuanza majibiazano ya risasi na askari ambapo kati yao watano walijeruhiwa na wengine saba walitoroka.
Kwa upande wake Saad Mtambule Mkuu wa Wilaya ya Mufindi amesema vitendo vya uhalifu katika Wilaya hiyo havina nafasi hivyo ametoa rai kwa wananchi kuacha vitendo vya uhalifu kwani hakuna mhalifu atakayesalia salama.