''Vijana wa UVCCM wanajipendekeza'' - Sosopi

Kupitia kipindi cha KIKAANGONI cha East Africa Television Mei 16, 2018, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Patrick Ole Sosopi, amesema vijana wa UVCCM wanafanya mambo kwa kujipendekeza ili wateuliwe

Sosopi amesema vijana wa BAVICHA wanafanya kazi ya kujitolea kutetea mambo mbalimbali nchini ikiwemo demokrasia na amani, kwasababu hawana malipo tofauti na UVCCM ambao wanafanya mambo kwa kujipendekeza ili wateuliwe kwenye nafasi mbalimbali serikalini.
''Kuna tofauti kubwa kati ya vijana wa CHADEMA na CCM kwasababu sisi hatuna mtu wa kumfurahisha, utamfurahisha Mwenyekiti Mbowe ili akupe nini, kwetu hakuna nafasi za uteuzi lakini wenzetu wanatazama kuwa DC, RC au DED'', ameeleza.
Sosopi ameongeza kuwa kitu pekee ambacho kina mjenga kijana wa BAVICHA ni 'struggle'. ''Ili uwe mbunge au kupata nafasi yoyote ndani ya Chama ni lazima 'ustruggle' hakuna njia nyingine''.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo