Mwaka 2002/04 tulikubaliana kati ya wadau wa vyama vya siasa na serikali tuwe na chuo cha Kitaifa cha kuandaa viongozi bila kuangalia itikadi za vyama kipindi cha Awamu ya Tatu Je, Serikali imefikia wapi katika kuandaa chuo hicho ili tuwe na taifa 1 lenye malengo yanayo fanana?
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde ambaye alijibu kuwa nia na dhamira ya serikali ni kuendelea kukuza demokrasia ndani ya nchini.
“Nia na dhamira ya serikali ni kuendelea kukuza demokrasia ndani ya nchi na makubaliano yaliyofanyika mwaka 2002-2004 tutaendelea kuyafanyia kazi na kufuatilia ili ombi hili liweze kutimia la kuwa na chuo cha kuwaweka wanasiasa. Tunaamini kupitia chuo hicho basi tutakuwa tumejenga taifa la watu wazalendo na wenye ari ya kweli ya kuwatumikia watanzania”, amesema Mavunde.