Rais Magufuli atamani Panya waweze kuwatambua waathirika wa Ukimwi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa amefurahishwa na Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine (SUA) cha mkoani Morogoro kwa kufanya utafiti wa panya kugundua bomu liko wapi.

Hali ambayo ilipelekea Rais Magufuli kusema kuwa chuo hicho kikiendelea hivyo hivyo anatamani panya waweze kumnusa mtu ili waweze kujua kama ana Ukimwi au hana.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Mei 7 alipotembelea chuo hicho, ambapo amesema kuwa anakipenda chuo hicho kwasababu ni chuo cha pekee.
“Moja ya tafiti za kipekee zilizofanywa na chuo hiki, ni ile kumfundisha panya namna ya kutegua mabomu na kugundua wagonjwa wa kifua kikuu. Hongereni sana SUA,” amesema Rais Magufuli.
“Utafiti ambao umeitangaza Sokoine ni ule wa kuyafanya mapanya kugundua mabomu yako wapi na pia kuweza kujua ni nani ana Kifua Kikuu, Najua mkiendelea hivyo mnaweza mkayatumia yakimnusa mtu yanajua nani ana UKIMWI hana.”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo