Picha 18: Mabasi Yakwama Makete, Angalia Ilivyokuwa

 Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Njombe kwenda Makete na wale wa Ikonda kwenda Njombe jana wamekwama kwa zaidi ya saa 5 kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kupelekea utelezi wa barabara


Magari hayo yamekwama katika kijiji cha Tandala kabla ya kunasuliwa na mitambo ya mkandarasi anayejenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami kutokana na magari hayo kukwama kwenye barabara mchepuko iliyotengenezwa na mkandarasi huyo

Zoezi la kunasua magari hayo limeanza saa 10 jioni na kumalizika saa moja jioni


 Msaidizi wa Askofu Dayosisi ya Kusini Kati, Mch. Adili Pagalo akionja adha ya kukwama






 Abiria wakishusha mizigo yao baada ya kukata tamaa ya kuendelea na safari




Basi la Mwafrika likivutwa majira ya saa moja Usiku ili linasuliwe kwenye mkwamo huo. Picha na Edwin Moshi wa Edmo Blog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo