Mchungaji adaiwa kumuua Mkewe kwa Kisu

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Rose Mndenye ameuawa kwa kuchomwa kisu na mume wake usiku wa kuamkia leo ambapo baada ya tukio hilo mume wake amekimbilia kusikojulikana.

Mhadhiri huyo wa chuo cha biashara katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Rose Mdenye ameuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe usiku wa kuamkia leo mei 26 huku sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Rose Mdenye ameuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe wa ndoa ambaye ni mchungaji wa Kanisa aitwaye John Mwaisango.

Tukio hilo limetokea kwenye nyumba yao mjini Dodoma.

Chanzo: mwananchi

Ofisa habari na uhusiano wa chuo kikuu hicho (UDOM), Beatrice Mtenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa taarifa zaidi zitatolewa baadae.

Mtenga amesema msiba upo Kisasa Sheli.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo