Mbunge Chadema augua ghafla

Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro imeahirisha kesi ya tuhuma za kuchoma ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Sofi baada ya mshtakiwa wa kwanza, Suzan Kiwanga kuugua ghafla.

Kabla ya kuhairishwa kwa kesi hiyo leo Alhamisi Mei 17, 2018, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali,  Sunday Hyera ulionekana kutokubaliana na taarifa hizo za ugonjwa.

Hali hiyo ilimfanya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Ivan Msack kumtaka mdhamini pamoja na wakili wa upande wa utetezi, Barthelomew Tarimo kuwasilisha taarifa ya daktari itakayothibitisha taarifa hizo za ugonjwa.

Wakili Tarimo na mdhamini wa Kiwanga walitoka na kwenda kuchukua taarifa hiyo ya daktari wa kituo cha afya cha Aga khan iliyoeleza kuwa Kiwanga anasumbuliwa na kichwa na maumivu ya mwili na kuiwasilisha mahakamani.

Katika taarifa hiyo ya daktari ilieleza kuwa Kiwanga amepumzishwa kwa saa sita na hivyo Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Mei 18 mwaka huu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo