Mtoto Anaekadiliwa Kuwa na Umri wa Miaka
Miwili Mwenye Jinsi ya Kiume Amekutwa Akiwa
amefariki kando ya Mto Mhangachi Katika
Uwanja wa Mpira wa Shule ya Sekondari Chief
Kidulile Wilayani Ludewa katika Mkoa wa
Njombe.
Kwa Mujibu wa maelezo ya Mashuhuda
waliojitokeza katika Tukio hilo wamesema kuwa
Mwili wa Mtoto huyo ulionekana Tangu Asubuhi
ya Leo Mei 24 mwaka huu 2018 Wakati
Wanafunzi Wa Shule ya Sekondari Chief Kidulile
wakifyeka Nyasi katika Eneo la Kuzunguka
Uwanja wa Mpira ndipo walipouona Mwili wa
Mtoto huyo Ukiwa Umeanza Kuharibika na Kutoa
Harufu kali.
Mashuhuda hao wamesema kuwa Marehemu
amekutwa akiwa hana Kichwa na Kushindwa
Kutambuliwa Kuwa Ni Mtoto wa nani na mwili
wake Umebaki kuanzia katika eneo la Shingo,
Kushuka hadi Miguuni ambapo Kichwa Chake
Kinaonesha Kuwa Kimebondwa na Kuchakazwa
Vibaya na Kusababisha Watu washindwe
Kuitambua Sura ya Marehemu.
Muda Mfupi Baadae baada ya Kupokea Taarifa
Kutoka kwa Wasamalia wema wakiwemo
Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Sekondari
Chief Kidulile Askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya
Ludewa walifika Katika Eneo la Tukio na Kujionea
Hali halisi ya Tukio hilo Ambapo Kaimu Kamanda
wa Polisi Wilaya ya Ludewa ASP Malimi N
Malimi Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio hilo na
Kusema Kuwa Chanzo cha Tukio hilo Bado
hakijafahamika Maramoja na Jeshi la Polisi
Linaendelea na Uchunguzi Sambamba na
Kuiomba jamii ya Ludewa Kutoa Ushirikiano
katika Kubaini Muhusika wa Tukio hilo.
ASP Malimi Amesema Kutokana na Marehemu
kutotambuliwa na Mwili wake Kuharibika
kwasasa Jeshi la Polisi wilaya ya Ludewa
linaendelea na Taratibu za Kisheria ikiwemo
kupata Kibali ili Mwili wa Marehemu uzikwe
kuanzia Kesho na endapo Ndugu wa Marehemu
watajitokeza Taratibu nyingine zitaendele.
Kwaupande wake Daktari Frank Mwambasanga
aliyeupokea na Kuufanyia Uchunguzi Mwili wa
Marehemu katika Hospital ya Wilaya ya Ludewa
Amesema Kuwa Marehemu alikuwa Jinsi ya
Kiume anakadiriwa kuwa na Umri wa Miaka
miwili na Kuongeza Kuwa Tukio hilo Linakisiwa
kutokea Siku tano zilizopita ambapo Sababu
huenda ikawa ni Ajali kwakuwa Mwili wa
Marehemu umekutwa ukiwa na Majeraha,
ambapo Baada ya Ajali hiyo Kutokea Huenda
Mhusika wa Tukio hilo akaamua Kuutelekeza
Mwili wa mtoto huyo.
Aidha Daktari Mwambasanga Baada ya Kuulizwa
na Mwandishi wetu Kuwa Inawezekanaje ikawa
Ajali na Kusiwepo taarifa zozote kutoka kwa
jamii za Kupotea kwa Marehemu, Daktari
Mwambasanga Alisema Kuwa Mtoto huyo pia
huenda alikuwa anatokea Nje ya Mji wa Ludewa
kwakuwa Baada ya Tukio hilo Kutokea Hakuna Mtu yeyote Ludewa aliyetangaza Au Kutoa
Taarifa Kuwa Amepotelewa na Mtoto.

