Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy ameuomba uongozi wa shule ya sekondari Mang’oto iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe ambayo iliunguliwa na bweni la wavulana kulipa bweni hilo linalojengwa upya jina la Makete Development Association (M.D.A) ambacho ni chama cha maendeleo Makete
Mh Kessy Ameyasema hayo wakati akipokea bati 150, saruji mifuko 100 na misumari ya bati kilo 10 iliyokabidhiwa na chama cha maendeleo Makete (MDA)
“Kwa kuwa MDA wamenifanyia surprise naomba na mimi niwafanyie surprise, niwaombe mkuu wa shule lile bweni linalojengwa upya mliite MDA kama njia ya kutambua mchango wao mkubwa walioutoa baada ya bweni hilo kuungua” amesema mkuu huyo wa Wilaya
Akijibu ombi la Mkuu wa wilaya, Mkuu wa shule ya sekondari Mang’oto Mwl. Bonaventure Mgaya amelikubali ombi hilo na kusema jina la M.D.A litafaa kuitwa bweni hilo kwa kuwa pia litasaidia wanafunzi kwenda na muda Tazama hapa Chini:-
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube