Matokeo ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Twaweza kuhusu masuala ya elimu nchini, yameonyesha kuwa, asilimia 87 ya watanzania waliohojiwa katika utafiti huo wapo tayari kulipia gharama za elimu ili kupata elimu bora.
Ripoti ya utafiti huo inaonyesha kuwa, takwimu zilikusanywa kutoka kwa watu 1,789 waliohojiwa katika mikoa ya Tanzania Bara.
Meneja wa Utetezi Twaweza, Anastazia Lugaba amesema utafiti huo uliopewa jina la ‘Elimu bora au Bora Elimu’ amesema idadi ya wananchi wanaotaka elimu itolewe bure imepungua kutoka 56% iliyokuwa mwaka 2005.
“Tunaelewa kwamba tumeelekeza watoto wapate elimu bure, japo tumeondoa michango na pia tumeondoa ada lakini changamoto kwenye sekta ya elimu zinaonekana kuwa ni nyingi na kubwa sana, kwasababu walimu ni wachache na wanafunzi ni wengi sana” amesema Lugaba.
