KIJANA Frank Joseph mkazi wa Mbezi jijini Dar ambaye anakabiliwa na shitaka la wizi baada ya kumuibia Bi. Seva Selemani, furushi la mahindi linalokadiriwa kuwa na kilo 20 na kisha kumganda kichwani, leo alitakiwa kupandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo ya Mlandizi mkoani Pwani lakini ilishindikana baada ya gari la Magereza lililotakiwa kumtoa Gereza la Mkuza alikohifadhiwa kumpeleka mahakamani kuharibika.
Hakimu wa mahakama hiyo, Nabwike Mbaba, aliitaja kesi hiyo mahakamani hapo lakini Mwendesha Mashitaka wa Mahakama hiyo, Sajenti Mohammed, alimwambia hakimu Nabwike kuwa askari magereza walishindwa kumfikisha mahakamani hapo baada ya gari lao kuharibika.
Kufuatia mshitakiwa huyo kushindwa kufikishwa mahakamani hapo hakimu Nabwike aliiahirisha kesi hiyo mpaka mpaka Mei 14 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Aliyegandwa na Kiroba Kichwani, Ashindwa Kufika Mahakamani
By
Edmo Online
at
Thursday, May 10, 2018