Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wenzie wahojiwe

Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, inatarajia kuwahoji mwanahabari Paschal Mayallah na wahariri wa gazeti la kila wiki, la Raia Mwema kwa madai ya kuchapisha habari inayodhalilisha bunge, Aprili 9 wiki hii.

Hayo yameelezwa leo Aprili 12 bungeni na Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyesema kuwa habari iliyochapishwa Aprili 9 ilidhamiria kuchafua hadhi ya bunge.

Hayo yamekuja baada ya mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga kuomba mwongozo wa Spika juzi Aprili 9, akihoji iwapo habari iliyoandikwa na gazeti hilo yenye kichwa cha habari “Bunge linajipendekeza?” haidhalilishi bunge.

Spika Ndugai leo Aprili 12, ameliambia bunge kuwa mwandishi huyo na wahariri watatakiwa kuhojiwa na kamati hiyo ya bunge.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo