Mwigulu ataka wakamatwe na wasiachiliwe

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameliagiza Jeshi la Polisi kuwatoza faini, kuwaweka ndani madereva na wasiachiwe mpaka pale watakapo wafikisha Mahakamani pindi watakapo wabaini wanaendesha vyombo vya moto kwa mwendokasi

Mwigulu ametoa kauli hiyo leo (Aprili 05, 2018) katika Mkutano wa 11 wa kikao cha Bunge cha tatu kilichofanyika katika mkoa wa Dodoma wakati akitoa taarifa ya ajali iliyotokea wilayani igunga jana kwa kuhusisha lori aina ya fuso na basi la abiria la kampuni ya city boys na kuua watu 12.
"Taarifa za awali tulizopewa kwamba chanzo cha ya ajali hiyo sio mashimo ya barabarani pekee yake bali ni mwendo kasi wa dereva wa fuso ambaye alisababisha kuligonga basi hilo hivyo naliagiza jeshi la polisi popote pale watakapomkamata dereva anatembea mwendokasi pamoja na hiyo ya kutoza faini, wamuweke ndani wasimuachie mpaka pale watakapompeleka Mahakamani ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa", amesema Mwigulu.
Pamoja na hayo, Mwigulu ameendelea kwa kusema "endapo dereva huyo akitoka Mahakamani na kama rekodi zake ni mwendokasi basi anyang'anywe leseni yake ili asiweze kuendelea kuendesha magari yanayosababisha ajali na kupoteza maisha ya watu kama hivi jana ilivyotokea".
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amewataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama wa barabarani kutafakari kwa nini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo