
Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi mfawidhi mwandamizi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza Wilbert Chuma, baada ya kuridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka, ambao ulidai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya Novemba 14 hadi 16, 2016, na kumtaka kwenda jela miaka 30 na kulipa faini ya shilingi laki 8.
Mara ya kwanza shauri hilo lilifunguliwa mahakamani mwaka 2016 katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana ambapo hakimu aliyekuwa anasikiliza alijitoa, baada ya kuwepo madai ya kupanga njama za kuharibu kesi, na mnamo Januari 2018, Rais John Magufuli aliingilia kati kwa kumuagiza mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella kufuatilia kwa karibu upelelezi, uendeshaji na hatima ya shauri hilo ili haki iweze kutendeka.
Baada ya hapo Mkuu wa mkoa aliingilia kati na kuanza upya uchunguzi, na ndipo ilipothibitika muhumiwa huyo alitenda kosa hilo, na ndipo mahakama kutoa hukumu yake April 5, 2018.
Afisa Mtendaji huyo alishtakiwa kwa kosa la kubaka na kulawiti mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka 12.