Ukichezea amani unachezea maisha yako – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa mtu akichezea amani ya nchi amechezea maisha yake

Rais Magufuli leo Machi 15, 2018 wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philips Moris International mjini Morogoro.
“Ukichezea amani unachezea maisha yako. Unaweza ukadhani wewe uko mbali ukafikiri haitakupata. Isipokupata wewe, itampata hata ndugu yako,” amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo Rais amezungumzia mashamba yanayofutwa ameeleza kuwa “Nilishasema mashamba yote yanayofutwa, wapewe wananchi bure, ni mali yao, walidhulumiwa tangu zamani kwa wakubwa fulani fulani kujimilikisha”.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo