Nchini Kenya mkoa wa Bonde la Ufa jeshi la polisi nchini humo limemkamata ndugu Mathew Lempurkel kwa tuhuma za kutaka kujinyonga.
Mbunge huyo wa zamani wa Laipikia kusini Ndugu Lempurkel amekamatwa baada ya tetesi kuwa alikuwa na mpango wa kujinyonga na kwa sababu ambazo hazikujulikana mara moja.
Kamanda mkuu wa polisi kaunti ya Laikipia Simon Kipkeu alidhibitisha kisa hicho na kudai kuwa uchunguzi zaidi unaendelea kufanywa ili kubaini chanzo kilichopelekea mbunge huyo kuwa na mawazo ya aina hiyo.
“Tunafanya uchunguzi kubaini kilichompelekea Lempurkel kutaka kujitoa uhai,sitaki kuzungumzia mengi kwa sasa ila nitawaarifu zaidi baadaye,” Kipkeu alizungumza na waandishi wa habari Kuzungumzia jambo hilo.
Hata hivyo,Kipkeu alisema kuwa Lempurkel atafikishwa mahakamani hapo jana Machi 14 au leo Alhamisi Machi 15 kujibu mashtaka dhidi yake.
Mathew Lempurkel alikamatwa hapo juzi na maafisa wa jeshi wa polisi baada ya raia wema kutoa taarifa za madai kuwa alitaka kujinyonga nyumbani kwake.
Mnamo july 2016 Lempurkel pia akikamatwa na kushitakiwa katika mahakama ya Nanyuki kwa kosa kuchochea wafuasi wake walioteketeza kituo cha polisi cha Rumuruti Julai 2016.
