Picha Zote Bweni la wanafunzi Korogwe lilivyoungua Moto

Moto umeteketeza bweni katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe iliyoko mkoani Tanga na kuwaacha wanafunzi hao katika hali mbaya kufuatia mshtuko wa kupoteza vifaa vyao vyote.


Moto huo ulitokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia leo wakati wanafunzi takribani 40 wanaoishi katika bweni hilo wakiwa darasani wakijisomea.


Hata hivyo licha ya moto huo kutekeza bweni, hakuna madhara ya kimwili kwa upande wa wanafunzi hao isipokuwa kwa wale waliopata mshituko na kuzimia ambao wamelazwa katika Hospitali ya Magunga na Majengo wilayani humo.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, chanzo cha moto kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.


Credit: GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo