Mkuu wa Mkoa atoa wiki mbili tu

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge ametoa muda wa wiki mbili kukamilishwa kwa mkandarasi wa mradi wa Umwagiliaji unaofadhiliwa na Mpango wa Chakula Duniani WFP, ambao ulitarajiwa kukamilika mwaka 2017 wilayani Chamwino

Maelekezo hayo ameyatoa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya Kilimo inayotekelezwa wilayani Chamwino itakayogharimu zaidi ya shilingi milioni 800 ambapo vijiji vitatu vinatarajia kunufaika na mradi huo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa muda uliobaki mkandarasi huyo hana budi kupelekea mafundi wote katika eneo la mradi ili kuukamilisha kwa wakati licha ya changamot zilizokuwepo hapo awali.
"Jitahidini kuanzia leo mtakuwa mmebakisha wiki mbili tu. Yaani piga ua nataka mradi ukamilike haraka iwezekanavyo. Wewe tafuta hata mafundi wako msiangalie kwamba mtapata nini sidianeni,  mafundi washirikiane na Injinia huu mradi ukamilike," Mahenge.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo