Mwenyekiti wa CHADEMA Makete ahamia CCM Leo


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kata ya Luwumbu wilayani Makete mkoani Njombe Hii leo ametangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi (CCM)
Mwenyekiti huyo Bw. Aram Medson Kyando akizungumza na Eddy Blog muda mchache baada ya kuhama CHADEMA, Amesema sababu zilizopelekea kujiuzulu na kuhamia CCM ni kuunga mkono Jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais John Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Taifa
Amesema akiwa upinzani tangu 2013 walikuwa wakipigia kelele mambo kadhaa yatekelezwe na serikali lakini sasa ameona yakifanywa kwa vitendo na Rais Magufuli hivyo haoni sababu ya yeye kuendelea kuwa upinzani
Akijibu swali la mwandishi wetu kuhusu kununuliwa hasa kutokana na wimbi la viongozi wengi wa CHADEMA Kuhamia CCM, amesema hilo halina ukweli na badala yake yeye hajanunuliwa bali anaukubali utendaji kazi wa Rais Magufuli katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu bure, afya na miundombinu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo