CCM Makete yaipokea Taarifa ya Ilani ya Uchaguzi Baada ya Kuikataa Ile ya Awali


Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Makete imeipokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Makete kwa mwaka 2017 iliyowasilishwa kwao hii leo

Taarifa hiyo imewasilishwa hii leo na Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy ambapo imeonesha utekelezaji wa ilani hiyo ya uchaguzi umekwenda vizuri na ndiyo maana imepokelewa na wajumbe hao

Katika taarifa hiyo Mkuu wa wilaya amesema wilaya imefanikiwa kutoa pembejeo za kilimo kwa wakulima kwa wakati, kujengwa ghala la kuhifadhia mazao katika kijiji cha Madihani, kuchanjwa ng'ombe 24,798 magonjwa hatari ikiwemo kimeta pamoja na ng'ombe 17,581 kupigwa chapa wilaya nzima

Taarifa hiyo pia imegusia utekelezaji wa ilani katika nyanja zote ikiwemo elimu, kilimo, afya, maji pamoja na miundombinu

Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Makete Ndugu. Langael Akyoo amewataka watendaji wa serikali kufahamu kuwa wao kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM sio hiari bali ni sheria inawataka kufanya hiyo

Naye mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Ndugu Ona Nkwama amewaambia watendaji wa serikali ambao ndio watekelezaji wa ilani kuwa kazi yao kubwa ndio hiyo lakini wajiepushe kuonesha mapenzi ya vyama ofisini


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo