Mwanajeshi aliyefukuzwa kazi akamatwa na Polisi huko Dodoma

Jeshi la polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa 14 wa makosa mbalimbali ya kiuhalifu wakiwemo matapeli waliojifanya kuwa ni maofisa ununuzi kutoka Jeshi la Wananchi wa Watanzania (JWTZ) na maofisa usalama wa Taifa

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema watuhumiwa hao walikamtwa kwenye mitaa mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wakifanya vitendo vya uhalifu baada ya kumtapeli mfanyabishara mmoja kiasi cha sh. Million 8.
Waliokamatwa katika tukio hilo ni Shaaban Kwiyela (58) Mkazi wa Kijiji cha Igunga Mkoani Tabora, ambaye alifukuzwa kazi kwa  utovu wa nidhamu tangu mwaka 1995 akiwa kikosi cha 36KJ Msangani Kibaha Mkoani Pwani akiwa na cheo cha sajenti lakini amekamatwa akiwa na mavazi ya cheo cha Kaptein.
Wengine ni Emmanuel Michael (45) mkazi wa Iringa, Juma Pesambili (33) Mkazi wa Sai Mbeya na Emmanuel Mwagonela (50) Mkazi wa Mtaa wa Ghana mkoani Mbeya.
Msikilize hapa chini Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muroto akitolea ufafanuzi zaidi juu ya tukio hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo