Miili ya watu yaokotwa katika mto Arusha

Watu wawili ambao ni wanaondoa wamefariki dunia katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha baada ya kuchukuliwa na mafuriko katika mto Piyaya Kata ya Piyaya wilayani humo

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Yusuph Ilembo amesema miili hiyo imeonekana leo majira ya asubuhi baada ya maji ya mto huo wa msimu kupungua.
Aidha, Kamanda Ilembo amewataja marehemu hao kuwa ni Ormins Sunguyo na mkewe Nembris Sunguyo ambao walikuwa na mtoto wa mdogo aliyefahamika kwa jina la Oloosukuta Sunguyo ambaye alinusurika kifo.
Kamanda Ilembo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi katika mkoa wa Arusha kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua na kuepuka kuvuka mito wakati maji yanafurika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo