Mbunge akamatwa kwa kupanga mauaji

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Laikipa Mshariki nchini Kenya Mathew Lempurkel, amekamatwa tena na polisi nchini humo, baada ya kuachiwa siku ya tarehe 12 machi, kwa tuhuma za kupanga mauaji

Kwa mujibu wa Polisi wa Laikipa Kaunti Kamanda Simon Kipkeu, bwana Lempurkel ambaye alikuwa mbunge kupitia chama cha ODM, atafikishwa mahakamani baada ya wapelelezi kukamilisha taarifa zao.
Lampurkel alikamatwa baada ya kutishia kukichoma moto kituo cha polisi cha Rumuruti, kwa lengo la kumtoa mtuhumiwa ambaye alikuwa mahabusu mwezi Julai, 2016.
Mahakama iliamua kuwa Lampurkel ana kesi ya kujibu juu ya vurugu alizofanya, na kisha kukamatwa tena kwa tuhuma za kupanga njama hizo za mauaji.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo