Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia Hadija Msangi, mkazi wa wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, kwa tuhuma za kumchinja mtoto wake, Hashim Ally Msuya mwenye umri wa miezi tisa, na kumuweka ndani ya mfuko wa salfeti kisha kuuficha mwili wake chini ya uvungu wa kitanda.
Kamanda wa polisi Mkoa wa kilimanjaro, Hammis Issah ameeleza kuwa tayari uchunguzi umeshafanyika na mwili wa mtoto huyo umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Aliongeza kuwa bado wanamshikilia mama huyo kwa ajili ya upelelezi ila inadaiwa kuwa ana sumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa akili.
