BAADHI
ya wananchi wa kijiji cha Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wameibua tena
hoja ya kutaka kunywa pombe wakati wa asubuhi siku za mapumziko huku baadhi
yao wakiunga mkono serikali ya kijiji
kufuata utaratibu uliopo.
Hoja
hiyo imeibuka jana Machi 22, katika mkutano wa kijiji cha
Tandala
Mkutano
huo umeongozwa na viongozi wa serikali
ya kijiji ambapo baaadhi ya wananchi waliuomba uongozi wa serikali ya kijiji
kuwacha wafanyabiashara wafungue mapema vilabu vya pombe siku za juma mosi na
juma pili kwa sababu ni siku za mapumziko
Wamewasisitiza
wananchi wa kata ya Tandala kuendelea kufuata kanuni na sheria za nchi huku wakisema
siku za jumamosi na jumapili vilabu vya pombe vyote vifunguliwe kuanzia saa
sita mchana kama serikali inavyotaka.
Wananchi
wengine wa Tandala wemeunga mkono kauli hiyo ya viongozi wao huku wakisema kwa
watumiaji wa pombe wafuate sheria za nchi kwani serikali haina mchezo na hilo.
Pia
wamesema hakuna kiongozi yoyote anaeweza kuwaambia wananchi wafanye jambo
ambalo ni kinyume na sheria.
Hivi
karibuni waandishi wetu walishudia mkuu wa kituo cha polisi Tandala akiwakamata
wanaofungua vilabu vya pombe wakati wa asubuhi.
Katika
mkutano huo mbali na hoja hiyo zimezungumzwa ajenda mbali mbali za maendeleo ya
kijiji, ikiwemo kusoma mapato na matumizi ambapo wananchi waliipokea taarifa
hiyo.
Bonyeza Play hapo Chini uipate kiundani:-
Bonyeza Play hapo Chini uipate kiundani:-
