Mwananchi Tito akichangia hoja kwenye mkutano huo
Diwani wa kata ya Matamba Mh. Epheli Ng'ondya akifafanua jambo
Afisa mtendaji wa kata ya Matamba akisoma taarifa hiyo
Wananchi wa kijiji cha Matamba kata ya
Matamba wilayani makete mkoani Njombe wamekataa kuipokea taarifa ya mapato na
matumizi ya ujenzi wa daharia katika shule ya sekondari Matamba iliyopo
kijijini hapo
Hayo yameibuka katika mkutano wa
diwani wa kata hiyo na wananchi wa kijiji hicho, ambapo wananchi wamehitaji
risiti zinazoonesha matumizi ya fedha hizo pamoja na mchanganuo wa kila kijiji
kimechanga vipi
Afisa mtendaji wa kata hiyo ndiye
aliyesoma taarifa hiyo ya mapato na matumizi kwa wananchi hao
Hali hiyo ikawafanya wananchi wahoji
baadhi ya mambo waliyoona hayakwenda sawa katika taarifa hiyo lakini wakakubaliana kuwa ujenzi wa daharia hiyo utaendelea na watashiriki lakini taarifa hiyo ije kusomwa tena upya
Diwani wa kata hiyo Mh Epheli Ng'ondya
akaungana na wananchi wake kuagiza maamuzi ya wananchi yafanyiwe kazi, lakini
amewaomba wananchi kuendelea na ujenzi wa daharia hiyo hata kama wameikataa
taarifa hiyo
Wananchi hao wakakubali kuendelea na
ujenzi wa daharia hiyo huku diwani huyo akiwaasa wananchi kuwaepuka viongozi wa
kisiasa wanaofika kwenye kata yake na kupiga siasa badala ya kufanya kazi kwani
muda wa siasa haupo na kwa sasa ni wakati wa maendeleo


