Kigoma: Daktari feki aliyetibu kwa muda wa miaka 10 akamatwa


Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma limemkamata daktari feki toka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilaya ya Kasulu ambaye amekuwa akifanya kazi za utabibu kwa zaidi ya miaka kumi katika Hosiptali mbalimbali hapa nchini.

Kamanda wa Polisi wa Kigoma Martin, amesema wamemkamata Daktari feki kutoka kambi ya Wakimbizi ya Nyalugusu Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma,ambaye anatuhumiwa kufanya kazi hiyo asio na taaluma nayo kwa muda wa mika kumi katika Hospital mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Daktari huyo feki amekamatwa akiwa na cheti cha kugushi cha Udaktari, amekamatwa na cheti cha kugushi cha mazoezi ya vitendo (internship) vilevile amekamatwa na cheti cha kugushi cha Usajili wa baraza la Madiktari la Tanganyika.

Ameshawa kufanya kazi katika Hospital ya St. Mary's iliyopo Karagwe mkoani Kagera 2007 - 2008, Hospitali Ndanda mission, Hospitali ya Feza, Hospitali ya maria stoppers Mwenge Dar Es Salaam. Baade akaajiriwa na Shirika la Redcross kuanzia mwaka 2016 July hadi alipokamatwa Mwaka 2018.

Imefahamika alishawafanyia Upasuaji watu wawili mmoja ilikuwa Upasuaji wa kujifungua na mwingine Upasuaji wa bandama. Wote hao Walipoteza Maisha.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo