Askari Polisi watatu wajeruhiwa vibaya katika ajali ya gari la Polisi na Lori

Askari watatu wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha gari la Polisi na Lori.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amesema kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Machi 8 katika barabara ya Tengeru-Arusha saa 9 alfajiri wakati gari la Polisi lililokuwa likisindikiza gari la Benki Kuu kupeleka fedha mkoani Tanga lilipogongwa na lori aina ya tipa.

Ajali hiyo iliwajeruhi askari waliokuwa katika gari hilo na dereva kuvunjika miguu yote na kuumia vibaya kichwani.

Kamanda Ilembo amesema kuwa, ajali hiyo ilisababisha majeruhi kwa askari wengine wawili kwenye gari hilo

Jeshi la Polisi linamsaka dereva wa lori ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo.

Chanzo: Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo