skip to main |
skip to sidebar
Diwani wa (ACT-Wazalendo) ajiuzulu na kuhamia CCM
Diwani wa Kata ya Gehandu Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara kupitia ACT-Wazalendo, Ndugu Mathayo Samhenda, leo Machi 3, 2018 amejiuzulu udiwani na kujivua uanachama wa chama chake na kuhamia rasmi CCM.
Diwani huyo amefanya hivyo ikiwa ni siku chache tu tangu amweleze LIVE Kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe kusudio la kuhama. Alifanya hivyo Februari 27 kwenye kikao cha ndani kilichofanyika wilayani Hanang na Zitto kuchukua maamuzi ya kumfukuza Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Manyara.
Diwani Samhenda amesema anajiunga na chama cha kweli cha siasa kinachoongozwa na Mzalendo namba moja Dr. John Pombe Joseph Magufuli na ameachana na vikundi vya harakati.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi