CHADEMA Hatarini Kutoweka, Makada wake wazidi kujiunga CCM

Tunduma. 
Hali imezidi kuwa mbaya kwa chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema, kufuatia viongozi na wanachama wake kuendelea kukihama chama hicho na kujiunga na chama tawala cha CCM.
Siku ya jana Jumamosi Machi 3, 2018, viongozi na wanachama zaidi ya 600 wa chama hicho wamejivua uanachama na kujiunga na chama cha CCM.
Kundi hilo linawajumuisha Katibu Mwenezi wa Chadema Jimbo la Tunduma, ndugu Liego Jackson, Shongola Mweka ambaye ni mweka hazina wa Chadema Jimbo la Tunduma, na ndugu Lazaro Ahonga ambaye ni Katibu wa Chadema wilaya ya Ileje.
Wengine ni ndugu Julius William ambaye ni diwani wa kata ya Sogea, na ndugu Frank Mwasandui Mponzi ambaye ni diwani wa kata ya Majengo, wote kutoka wilaya ya Tunduma.
Viongozi hao na wanachama wa Chadema walipokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, ndugu Humphrey Polepole alipokuwa kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya ya Tunduma.
Kwa siku za hivi karibuni, viongozi na wanachama kutoka vyama vya upinzani, ikiwemo Chadema, wamekuwa wakivihama vyama vyao na kujiunga na CCM ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli.
Wamekuwa wakitoa sababu za kuchoshwa na ubabaishaji uliopo kwenye vyama hivyo vya upinzani, huku wakidai kuwa vyama hivyo havina ajenda yoyote ya maendeleo kwa taifa zaidi ya kupigania maslahi yao binafsi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo