Atakayefanikisha kukamatwa dereva kupandishwa cheo

Jeshi la Polisi mkoani Pwani limeanzisha kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kufuatilia madereva wanaowashawishi askari kupokea rushwa pindi wanapokutwa na makosa ya usalama barabarani na kuahidi kuwa litawapandisha vyeo askari watakamata dereva hao

Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Pwani Jonathan Shana, amewaambia waandishi wa habari kuwa huo ni mkakati mmoja wapo wa kupambana na ajali za barabarani mkoani humo.
Aidha Kamanda Shana amefafanua kuwa kikosi kazi hicho ambacho kinaundwa na makachero kimeshaanza kazi na hatua za kisheria zitachukuliwa mara moja kwa madereva watakaokutwa na makosa hayo ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Kamanda Shana amesema mkakati huo wa kupunguza ajali pia utalenga kuwafungia leseni pia kutangaza kwenye vyombo vya habari makampuni  yote ya mabasi ambayo yatakuwa yamekithiri kwa makosa ya mwendo kasi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo