Tumemaliza ziara yetu ya kutembelea Kata ya Kikeo, inayoongozwa na Diwani wa chama cha ACT Wazalendo, hapa Halmashauri ya Mvomero, mkoa wa Morogoro.
Tumewashukuru wananchi kwa kuchagua Diwani wa Chama chetu, tumewasikiliza kero, matarajio na changamoto zao, tumemsikia diwani wetu, jitihada zake kushirikiana na wananchi wenzake kujiletea maendeleo, tumekagua kazi anayoifanya, tumeiona miradi yao, tumeshauriana na Diwani pamoja na wananchi, tumewapongeza kwa hatua mbalimbali walizochukua, pamoja na kuahidi kusaidiana nao kutatua changamoto walizonazo katani. Ziara yetu imekuwa nzuri.
Polisi wametuvamia jioni hii, hawajatueleza wanachokitaka. Tunakwenda nao kituo cha Polisi Mgeta muda huu kuwasikiliza.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Februari 22, 2018
Kikeo
Mvomero
Morogoro
