Baadhi ya waombolezaji ambao walijitokeza kuaga mwili wa marehemu Akwilina aliekua anasoma katika Chuo Cha Usafirishaji (NIT ) jijini Dar es Salaam wamepokonywa mabango mbalimbali ambayo yalikuwa na jumbe mbalimbali kuhusiana na kifo hicho
Waombolezaji hao ambao wengine walikuwa wameshika mabango kuhoji uhalali wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba na IGP Sirro kuendelea kuwepo ofisini mpaka sasa licha ya mauaji hayo kutokea.
Walijitokeza vijana mbalimbali ambao walikuwa wamevaa suti nyeusi na kuanza kupokonya mabango hayo kwa waombolezaji hao na kuondoka nayo, tukio hilo limetokea wakati Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako akihutubia mamia ya waombolezaji katika Viwanja vya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT).
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi