Wanahabari hawa Kujisalimisha kwa DCI

MAHAKAMA Kuu iliamuru wanahabari watatu wa kampuni ya Nation Media Group wanaosakwa na polisi wafike katika makao makuu ya uchunguzi wa jinai (DCI) Jumatatu.
Jaji Luka Kimaru alitoa agizo hilo alipowaachuli ) Linus Kaikai, Larry Madowo na Ken Mijungu kwa dhamana ya Sh100,000.

Jaji Kimaru aliwataka watatu hao wasichelewe kufika katika afisi za DCI wakiandamana na mawakili wao.
Watatu hawa waliwasilisha kesi chini ya sheria za dharura Alhamisi wakiomba Mahakama izuie serikali kuwakamata na kuwazuilia pasipo na sababu.
Wanahabari hawa walisema katika kesi waliyomshtaki Mwanasheria Mkuu (AG) kwa niaba ya Inspekta Jenerali (IG), DCI na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) wanasema wamekuwa wakiandamwa na maafisa wa polisi kwa lengo la kuwatia nguvuni na kuwafungulia mashtaka wasioyajua.
Mabw Linus Kaikai, Larry Madowo na Ken Mijungu wanapinga hatua yoyote ya kuwashtaki.
Watangazaji hao walimweleza Jaji Kimaru kwamba, “polisi wamekuwa wakipiga kambi nje ya jumba la Nation Centre, lililoko barabara ya Kimathi, Nairobi".
Walalamishi hao waliambia mahakama kwamba, Waziri wa Usalama Dkt Fred Matiang’i alisema alipokuwa anafunga vituo vinne vya televisheni kwamba, “Polisi watachunguza mchango wa baadhi ya wanahabari katika njama za kuihujumu na kuipindua Serikali.”
Wanahabari hao walisema matamshi hayo ya Dkt Matiang’i yanalenga kuwaharibia sifa na kuwasawiri kama wahusika wakuu kwenye utekelezaji wa madai ya Dkt Matiang’i.
Dkt Matiang’i aliagiza vituo vya televisheni vya NTV, KTN News, Citizen TV na Inooro vifungwe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo