Wanachuo wavamiwa na kubakwa

Polisi katika eneo la Embu Magharibi nchini Kenya, wameanzisha uchunguzi wa tukio la kubakwa kwa wanafunzi watano wa vyuo, baada ya kuvamiwa na kundi la vijana takriban 10 na kuwaibia mali zao na kisha kuwabaka

Wanafunzi hao ambao wanaishi hostel huku wakiwa wa vyo tofauti vya Chuka University, Chuo Kikuu cha Embu, Chuo cha mafunzo ya Madawa cha Kenya, walivamiwa na kundi la vijana wakiwa na mapanga usiku wa Februari 2 katika eneo la Bondenu huko Embu, na kuwapora vitu vyao kabla ya kuwachukua watano na kwenda kuwabaka.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mmoja wa wanafunzi hao ambaye jina lake halikuwekwa wazi, amesema kwamba watu hao walipoingia hostel usiku, walichukua simu, pesa, laptops, mitungi ya gesi na vitu vingine vya thamani, na kisha kuwafanyia kitendo hicho cha kikatili.
Hostel hiyo ambayo iko umbali wa mita 100 kutoka kituo cha polisi cha Embu Magharibi, waliingiwa na hamaki baada ya kuona simu zao hazipokelewi, na hata majirani hawausikia kelele zao.
Kamisha wa Kaunti ya Embu Esther Maina amesema tukio hilo limechelewa kupatiwa msaada wa kipolisi licha ya kuwa karibu, kutokana na polisi hao kuwa wamelala wakati wa kazi, na kwamba wanafunzi hao wamepekwa hospitali kwa matibabu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo