VIDEO: Kama hawachangi, watoto wao hawatakula - Wananchi Ikonda


Wananchi wa kijiji cha Ikonda wilayani Makete mkoani Njombe wameazimia kwa kauli moja watoto wao waendelee kupata chakula shuleni
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika hii leo kijijini hapo ambao ulikuwa na ajenda mbalimbali, pamoja na mambo mengine umejadili suala la wanafunzi wa shule ya Msingi Ikonda kupata chakula shuleni
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Alexander Mbilinyi ametoa fursa kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo Mwl Enerika Kayombo kutolea ufafanuzi kwa nini suala hilo la chakula limeletwa katika mkutano wa kijiji kujadiliwa
Baadhi ya wananchi wamelizungumzia suala la watoto kupata chakula shuleni na kusema suala hilo halikwepeki
Kufuatia majadiliano ya muda mrefu mkutano huo kwa pamoja umeazimia Jumatano ya wiki ijayo Februari 7 mwaka huu, wazazi wa wanafunzi wote wa shule hiyo wakutane kwenye mkutano maalum ambao pamoja na mambo mengine suala la chakula litajadiliwa Kama anavyosema mwenyekiti wa kijiji Alexander Mbilinyi
Katika hatua nyingine Kaimu Afisa mtendaji wa kata ya Tandala ambaye pia ni Afisa mtendaji wa kijiji cha Tandala Bw. Robert Nnko ameipongeza shule ya msingi Tandala kwa kufanya vizuri katika matokeo ya Darasa la saba Mwaka jana Wakati huo huo taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji hicho tangu Oktoba 2017 hadi januari 2018 imesomwa katika mkutano huo
Taarifa hiyo imesomwa kwa wananchi hao na Mwenyekiti wa kamati Bw. Adenusi Mbilinyi, taarifa ambayo imepokelewa na wananchi hao

tazama Video Hii>>>>>>


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo