Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, Msukuma amesema anashangazwa na watu wa tafiti na madaktari wanaokataza matumizi ya bangi na kuruhusu pombe kama viroba, ambazo zina madhara makubwa kwa afya zao.
“Lengo langu, mimi natoka kijini ambako kiukweli watu wanavuta bangi naona na wanalima tu, nilichokuwa nakisema nilikuwa nasema kama muwakilishi, ninaona maisha ya kule vijijini, vijana wetu walikuwa wakinywa viroba vitano tu wanaanza kujikojolea na kunya na kulala barabarani, lakini akila bangi ya shilingi mia tano tu hata kama ni saa 10 jioni, anaenda kulima mpaka saa 4, sasa nikawa nauliza hawa watu wa research maprofesa na madaktari, unazuiaje bangi ambayo mtu anavuta anaenda shambani, halafu unaruhusu kiroba ambavyo mtu akinywa viwili unajinyea”.
Mbunge huyo ambaye pia ni kijana sio mara ya kwanza kuibuka na kutetea hoja hiyo ambayo alianzia bungeni, na kuibua hisia kubwa kwa watu mbali mbali kwani inafahamika kuwa matumizi ya bangi si salama.
