Halmashauri ya wilaya ya Makete kupitia idara ya afya kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la (JHPIEGO) limedhamiria kuendesha zoezi la tohara kwa wanaume wenye umri wa miaka kumi na kuendelea bila malipo katika kata za UKWAMA na IPEPO kwa lengo kupunguza athari zinazowakumba wasiotairiwa kama maambukizi ya VVu na saratani ya shingo ya kizazi kwa wenza wao
Akizungumza na mwandishi wetu mratibu wa UKIMWI kutoka idara ya afya DK SHINGULE MWAMBALE amesema zoezi hilo litafanyika hivi karibuni katika kata za UKWAMA na IPEPO katika vijiji vya UTWEVE, MASISIWE, UKWAMA, IPEPO, MALIWA na IKETE ambapo zoezi hilo litaendeshwa bila malipo kwa waume wenye umri kuanzia miaka 10 na kuendelea
Mwambale pia ameelezea umuhumu wa tohara kwa mwanaume huku akiwaasa wakazi wa kata hizo kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma hiyo itakayofanyika kwenye zahanati za vijiji na ofisi za vijiji kwa maeneo yasiyo na zahanati
Na Riziki Manfred