Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa mtu mmoja aliyehusika na kumbaka hadi kufa mtoto wa miaka 5, kiongozi mmoja wa kidini kwa kosa la kumkatisha masomo na kumpatia ujauzito Mwanafunzi na kumzalisha watoto 2, watendaji, Maofisa mikopo wa mabenki na madalali wanaogushi nyaraka na kuwatapeli nyumba na ardhi wananchi wa mkoa huo.
Pia ameagiza kusimamishwa kwa shughuli zote za mabaraza ya kata mkoani humo pamoja na kesi zote hadi hapo utaratibu wa kupitia upya taaluma za wanasheria waliopo katika mabaraza hayo utakapofanyika.
Makonda ametoa maagizo hayo wakati akipokea ripoti yenye taarifa za malalamiko ya wananchi yaliyowasilishwa kwa jopo la wanasheria wapatao 409 kuanzia tarehe 29/01/2018 hadi tarehe 3/02/2018 mkoani humo ambapo zaidi ya wananchi elfu 11 walijitokeza kuwasilisha changamoto zao mbambali.
Miongoni mwa changamoto zilizo wasilishwa kwa wanasheria hao nipamoja migogoro ya Ardhi, Makosa ya Jinai, Miradhi, Malezi ya mtoto, Madai, Kulalamikia taasisi za kifedha na kibenki, kucheleweshwa kwa fidia, Manispaa zote za jiji hilo zimelalamikiwa kwa ukiritimba, Taasisi za bima, Mikataba ya mauziano kukiukwa, Watendaji wa serikali za mitaa kuuza viwanja kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja, kesi zinazoendelea mahakamani, Mahakama za mwanzo kutotenda haki, na Wananchi kukosa imani na jeshi la polisi na watendaji wa serikali.
Akizungumzia sakata la kubakwa hadi kufa kwa mtoto wa miaka 5 Mwanasheria Janet Eden amesema kuwa tukio hilo lilitokea mwaka mmoja ulipita lakini hadi leo, Polisi wa kituo cha Sitakishari Wilaya ya Ilala kulikoripotiwa kesi hiyo wameshindwa kufungua kesi, kumchukulia hatua mbakaji licha ya mama wa mtoto huyo kuangaika kupata haki yake, na ikaelezwa kuwa hata mama wa mtoto huyo alipo jaribu kumpelea mtoto Hosptali pia alinyimwa matibabu hadi mtoto huyo kufariki dunia.
Kufuatia sakata hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ameagiza kukamatwa kwa mbakaji huyo na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya aliyembaka na askari walioshindwa kuchukua hatua za kisheria kwa mbakaji, ili mlalamikaji apatiwe haki yake ya kisheria.
“Polisi anashindwa kumkamata mbakaji aliye mbaka mtoto hadi kumsababishia kifo, kwa bahati mbaya mama yule hata Hosptalini akanyimwa matibabu kwa mtoto wake atuwezi kuwa na Polisi ambao wanaharibu sifa ya serikali, kituo cha Polisi Sitakishari nilazima tupate majibu ya masuala haya, nashangaa hata Polisi wa kituo cha Oysterbay wanalalamikiwa kushiriki uuzwaji wa magari ya kitapeli ambapo gari mmoja linauzwa kwa watu 6 mfululizo, nilazima tuyashugulikie” amesema.
Wakati huo huo, Mhe Poul Makonda amekosoa utendaji wa mahakama ndani ya mkoa wa Dar es Salaam, ambapo ripoti imeonyesha Mahakamani kugubikwa na dhuluma, kuchelewesha haki, mahakimu kuwatishia wateja wao, kupotea kwa mafaili na nyaraka, kutumika kwa lugha ya kiingereza katika kuendesha kesi kiasi cha kuwanyima uelewa walengwa, na Rushwa iliyokidhiri katika mhimili huo.
“Sijui niwapeleke wapi wananchi wakapate haki kama taasisi nyeti ambazo zingesimamia haki zinawanyima haki, Kuaniza serikali za mitaa hadi ngazi ya Halmashauri wanaminya haki, Jeshi la polisi wamepoteza imani nalo alikadhalika Mahakama, sasa najiuliza nipeleke wapi kero za wananchi hawa I’ll zitatuliwe? ”Amehoji
Mbali na masuala hayo pia Makonda aliagiza kuondolewa kwenye nyadhifa zao baadhi ya watendaji 3 wakiwemo wakuu wa idara za ardhi za manispaa ya Ilala na Temeke, kwakushindwa kusimamia ipasavyo majukumu yao ya kikazi.
Pia ameahidi uhakikisha kuwa wananchi wote waliodhulumiwa haki zao wanapatiwa haki, na kwa wale ambao kesi zao zinapaswa kusikilizwa mahakamani watapewa wanasheria bila malipo ili kuhakikisha wanapata haki zao kwa wakati.