Richard Hizza Tambwe Kuzikwa Kesho Dar


MWILI wa Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Richard Tamilway maarufu kwa jina la ‘Tambwe’ aliyefariki dunia jana asubuhi nyumbani kwake Mbagala Kizuiani, unatarajiwa kuzikwa kesho Jumamosi katika Makaburi ya Temeke Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Global Publishers, kaka wa marehemu aitwaye Charles Tamilway amesema kuwa taratibu za kuuhifadhi mwili wa kaka yake katika nyumba yake ya milele zinaendelea kufanyika na kama ratiba isipobadilika, mwili huo utahifadhiwa kesho Jumamosi kama ilivyopangwa.

Naye mjane wa marehemu, Mariamu Masoud, alisema  mume wake hakubahatika hata kufika hospitali kupata matibabu ya kuokoa maisha yake baada ya kuugua ghafla, hivyo anamuomba mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mumewe mahali pema peponi.

Hizza anafahamika sana kwa siasa zake akiwa Chama cha Wananchi (CUF), baadaye akahamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa chama hicho na mwaka 2015 aliamua kuondoka CCM na kuhamia CHADEMA.
 Kulia ni mtoto wa marehemu, Agnes Richard akifarijiwa
Habari: Brighton Mwasonya na Denis Mtima/Gpl


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo