Uteuzi huo umefanyika leo ambapo kupitia taarifa ya Wizara hiyo imeeleza kuwa Waziri Mwakyembe amepewa mamlaka ya kufanya hivyo na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha Mwakyembe pia ameteua wajumbe wapya sita wa Baraza hilo pamoja na wajumbe wengine watatu ambao wataongoza nafasi mbalimbali ndani ya Baraza hilo kama taarifa hapo chini inavyoeleza.
Tenga aliongoza Shirikisho la soka nchini kwa awamu mbili kabla ya kuachia nafasi hiyo ambapo mwaka jana pia aliteuliwa na Shirikisho la soka Barani Africa (CAF) kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho hilo.